HEALTHY VILLAGERS CAMPAIGN

TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU CALL: 0712 005 865 au EMAIL: dr.masua@paulmasua.com

Wednesday, March 20, 2013

Maambukizi ya fangasi sehemu za siri(Vulvovaginal candidaiasis)Candida ni aina ya fangas wanaoweza kuathiri sehemu mbalimbali ya mwili wa binadamu. Mara nyingi hushambulia sehemu laini za mwili (mucuos membrane), pia wanaweza kuathiri ngozi na kusambaa kwenye damu hasa kwa wagonjwa wenyewe upungufu wa kinga. Katika makala haya tutaangalia maambukizi kwenye sehemu za siri za mwanamke(vulvovaginal candidaiasis)


Zaidi ya asilimia 78 ya wanawake hupata maambukizi ya  fungus sehemu za siri mara moja au zaidi katika maisha. Hata hivyo baadhi hupata maambukizi  mara kwa mara.Maambukizi hufanya na aina ya fangas waitwa Candida albicans. Fangasi hawa kwa kawaida hupatika katika njia ya uzazi ya mwanamke(kuma) bila madhara yoyote, lakini hali inapobadilika huweza kusababisha ugonjwa. Hata hivyo haijulikani ni mabadiliko gani huweza kuchochea hali hii kutokea lakini mabadiliko ya hormone yanahisiwa kusababisha.

DALILI
Ugonjwa huu unaweza kuwa na dalili mbalimbali 
Mgonjwa anaweza kusikia miwasho, kuchubuka sehemu za siri, kusikia maumivu wakati wa kujamiiana au wakati wa kukojoa na pia kutoa uchafu mweupe kama maziwa mgando ambao kwa kawaida hauna harufu.
Pi dalili hizo zinaweza kuambatana   na kuvimba mashavu ya njia ya uzazi, kidonda au mipasuko.

UCHUNGUZI
Ugonjwa huu unaweza kujulikana kwa njia ya hadubini(microscope),kuotesha ( culture) na antigen.

MATIBABU
Dawa za aina tofauti zinaweza kutumika kutibu ugonjwa huu.. Dawa zinaweza kuwa za kutumbukiza kwenye njia ya uzazi wa mwanamke(suppositiries) au za kupaka(cream). Wakati mwingine mgonjwa anaweza kuandikiwa dawa za kumeza iwapo amekuwa akipata ugonjwa huu mara kwa mara.

5 comments:

 1. Mimi ninaugonjwa kama huo uke uliowekwa hapo, huwa natoa fangasi nyeupe hivyo hivyo, nimetumia dawa lakini kila baada ya muda zinarudi, jee nitumie dawa gani?

  ReplyDelete
 2. pole sana kwa tataizo linalokusumbua. unaweza kunicheki kwenye hii email kwa maelezo zaidi drmasua@paulmasua.com au paulmasua@gmail.com

  ReplyDelete
 3. clinic yako ipo wap.mimi nataka kucheck afya yangu kwa upande wa uzazi kiujumla

  ReplyDelete
 4. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete