Waziri wa mashauri ya kigeni wa US Hilary Clinton anaendelea vizuri kufuatia kupatikana na tone la damu kwenye mshipa mmoja wa kichwa, lakini hata hivyo hakupata kiharusi(stroke) wala madhara mengine kwenye mfumo wa fahamu. Madaktari wanaomtibu wamesema wanauhakika atapona bila matatizo yoyote.
Katika taarifa iliotolewa na madaktari imesema tone hilo la damu iliyoganda liko kwenye mshipa uliko kati ya ubungo na fuvu la kichwa nyuma ya sikio la kulia. Anapewa dawa za kuyeyusha damu na ataendelea kubaki hospitali.
Imeelezwa kuwa madaktari walibaini tatizo hilo ktk uchunguzi wa kwaida wa afya kufuatia kupata mtikisiko wa ubongo mwanzoni mwa mwezi december. Bi Clinton anatarajiwa kuachia wadhifa alionao mwezi huu.Hata hivyo haijajulikana kama atagombea tena ktk chama chake hapo baaadae.
Wkati huo huo rais wa Venezeula Hugo Chaveza afya yake imeendelea kuwa tete kufuatia kupata maradhi zaidi katika mapafu yake zikiwa zimepita wiki tatu tangu afanyiwe operation ya kuondoa uvimbe maeneo ya nyonga. Jana raia wa Venezuela wakiongonzwa na baraza la mawaziri wamefanya ibada ya kumuombea. Chavez anatarajia kuapishwa tarehe 10 mwezi huu. Amekuwa akipata matibabu ya saratani nchini Cuba na ameisha fanyiwa operation nne.
No comments:
Post a Comment