Leo ni siku ya mwisho ya mwaka 2012. Napenda kumshukru Mwenyezi Mungu kwa nguvu na ulinzi aliotujalia ktk mwaka huu wote. Lakini pia nimshukru kwa ujasiri aliotupa wa kutumiza malengo na ahadi zetu. Kuna ndugu zetu wengi walipoteza maisha mwaka huu kwa sababu mbalimbali hao tunawaombea pumziko la amani. Wakati huu unaposoma hizi salaam kuna wengine wako vitandani kwa sababu mbalimbali, tuwaombee pia watumie dawa zao ili waweze kupona.
Ndugu zangu mwaka huu kuna mambo mengi yalitokea,mengine yalikuwa kwa sababu zetu na nyingine zilikuwa nje ya uwezo wetu. Lakini hayo sasa yamepita. Tunaanza upya. Tukiwa na malengo na ahadi mpya. Tufanye kazi kwa bidii ili tuweze kuyatimiza yale tunayojiwekea. Bila kujituma hatuwezi kupata mafanikio.
Lazima tujitahidi kujikinga na magonjwa kama inavyoelekezwa na wataalamu wa afya hii ikiwemo kufuata kanuni bora za afya,kuzingatia mazoezi na mlo kamili lakini pia kutafuta huduma na kufanya uchunguzi wa afya kadri ya muda na mahitaji. Uhai tulionao ni zawadi na tunao mara moja tu. Tujitahidi kulinda utu wetu na wa wenzetu ili kutunza uhai.
Masua Blog ya afya.
Nawashukru pia kwa namna mlivoipokea hii blog. Blog ambayo lengo kubwa ni masuala mbali ya afya yanayoathiri ustawi wa mwanadamu. Tumejipanga kuiboresha na kuifanya iwe karibu na wewe ndugu msomaji. Hata hivyo mchango wako bado ni wa muhimu ili kufanikisha kuboresha hii blog. Tegemea mabadiliko makubwa kuanzia mwakani (2013). Mawazo yako yanakaribishwa ili kusaidia kuboresha zaidi hii blog.
Kwanamna ya pekee ningependa kuwashukru watu wafuatao kwa michango yao ambayo imefanya blog hii iwe hivi:mke wangu Bi Lulu P. Masua, Sister Pendo Said, Dr. Adarick Makome, Dr. Joseph Obedi, Dr. Norbert Muna na Bw. Nicolaus Trac kwa kusaidi kuipa hii blog muonekano mpya.
Mwisho nakutakia fanaka za mwaka mpya 2013.
Asanteni wote.
Dr.Paul Masua

No comments:
Post a Comment