HEALTHY VILLAGERS CAMPAIGN

TANGAZA HAPA CALL 0712 005 865

Thursday, December 27, 2012

Mwanamke mjamzito hung'wata zaidi na mbu.


Mwanamke anapokuwa na ujauzito anaongezeka uzito pamoja na unene lakini pia anapumua kiasi kikubwa cha hewa ya ukaa(CO2).Hizi ni sababu zinazosababishwa mwanamke kufuatwa na mbu kwa urahisi zaidi. Tafiti zimeonyesha kuwa mjamzito anang'wata mara mbili zaidi kuliko mwanamke asiye kuwa mjamzito.
Sababu zingine zinazochangia mjamzito kung'wata na mbu ni kuongezeka kwa joto ridi la mwili. Kuongeza kwa joto la mwili hufanya kemikali kuyeyuka kwa urahisi na hivyo kufanya mbu kuvutiwa. Kuna kemikali za aina tofauti ktk mwili wa binadamu zinazoweza kuwavutia mbu.
Malaria ni ugonjwa mmojawapo unaosabambazwa n mbu. Ugonjwa huu huwashambulia zaidi kina mama wajawazito. Sababu hizo zinachangia mbu kuwang'wata zaidi.
Kuuangamiza mazalia ya mbu, kina mama wajawazito kutumia dawa za SP na kutumia vyandarua vilitiwa viuatilifu kama NGAO itasaidia kuwakinga kina mama na malaria.

No comments:

Post a Comment