Tukiwa ukingoni mwa mwaka 2012 ni vyema tukajikumbusha matukio mbalimbali yaliyotokea katika sekta ya afya. Haya ni baadhi ya mambo yaliyotokea mwaka huu.
1.Mgomo wa madaktari
Madaktari waliitisha mgomo tanzania nzima ulioduma kwa majuma kadhaa mwezi februari na juni. Lengo kuu la mgomo lilikuwa ni kuishinikiza serikali kuboresha huduma za afya pamoja na maslahi ya wahudumu wa afya. Mgomo huu ulisababisha baadhi ya madaktari kusimamisha.
Dr. Ulimboka alitekwa,kuteswa na kuumizwa vibaya kisha kutupwa katika msitu wa Mabwepande. Hili lilikuwa ni pigo kwa taaluma ya Afya lakini pia lilionesha uhai wa mtu usivyokuwa na thamani kwani mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa licha ya baadhi ya wahusika kutajwa.
3.Uzinduzi wa jengo la magonjwa ya moyo.
Mwaka huu tumeshudia uzinduzi wa jengo la kisasa la magonjwa ya moyo katika hospitali ya Taifa. Huduma hii itasaidia kupunguza wagonjwa kwenda nje ya nchi lakini pia wagonjwa kupata huduma za kisasa na za haraka.
4.Vifo vya madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya watoto.
Idara ya upasuaji wa magonjwa ya watoto ilipata pigo kubwa baada ya madaktari wake wawili kufariki dunia. Madaktari hao Dr. Swai na Prof. Carneilo walifariki dunia mwaka huu kwa nyakati tofauti hivyo kuacha idara hiyo ktk hali mbaya.
5.Tamko la serikali juu ya madaktari waliosimamishwa wakati wa mgomo.
Serikali imetoa tamko la kuwarudisha kazini na wengine kupewa adhabu kufuatia mgomo uliotokea mwezi juni.
6.Dawa za bandia za kukata makali ya HIV.
Kiwanda cha kutengeneza madawa
cha TPI kilituhumiwa kutengeneza dwa zisizokuwa na ubora hivyo kupelekea kufungiwa, hata hivyo wamiliki wa kiwanda hicho walikana kiwanda chao kuhusika na tuhuma hizo.
7.Uzinduzi wa chuo kikuu kishiriki cha Udaktari mkoani Songea.
Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino kilichoko jijini Mwanza kilizindua kilizindua chuo cha udaktari mkoani songea.
8.Serikali kujenga hospitali nyingine ya kisasa.
Ahadi hiyo ilitolewa na rais Kikwete wakati akizindua hospitali ya wilaya ya Temeke. Pia rais alisema hospitali hiyo itakuwa kubwa kama muhimbili na itakuwa na chuo cha afya. Hospitali hiyo itajengwa katika jiji la Dar es Salaam eneo la Mloganzila
9.Kuongezwa kwa chanjo.
Mwaka huu tumeshuhudia chanjo mbili za kuzuia magonjwa ya kuhara na homa ya mapafu zikiongozwa katika utaratibu wa chanjo za kitaifa.
10.Kifo cha Steven Kanumba
Mwezi April mwaka huu tasnia ya sanaa ilipata pengo kufuatia kifo cha msanii huyo. Taarifa ya uchunguzi wa madaktari ilieza kifo hichi kilisababishwa na mtikisiko wa ubongo
Nini kitatokea mwakani.??

No comments:
Post a Comment