Kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bacteria(Trapenoma pallidum s.pallidum). Ugonjwa huu unaweza kuathiri sehemu mbalimbali za mwili. Namna ugonjwa huu unavyoambukizwa inaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa mengine ya zinaa kama HIV.
Dalili za kaswende.
Dalili za ugonjwa huu zinategemea hatua(stage) ya ugonjwa. Kuna hatua tatu za kasendwe
Hatua ya awali(Primary stage)Dalili za ugonjwa huu zinategemea hatua(stage) ya ugonjwa. Kuna hatua tatu za kasendwe
Dalili za awali ni kidonda kidogo kigumu cha mvirongo kisichokuwa na maumivu sehemu za siri, mkundu au kwenye mdomo. Kwa kuwa kidonda hiki kinakuwa hakiumi mara nyingi hakichukuliwi hatua yoyote. Hatua hii hudumu kwa wiki tatu mpaka sita na kipele hupona chenyewe. Mgonjwa aliyeko katika hatua hii anaambukizi zaidi. Iwapo mgonjwa hakupata matibabu ugonjwa huendelea katika hatua ya
Hatua ya pili
Hatua ya mbali( late stage).
Hatua hii hufuata baada ya hatua hizo hapo juu kuwa zimekwisha. Endapo mgonjwa hakutibiwa huendelea kuw na wadudu kwenye damu hata kama hana dalili. Dalili zake ni kushindwa kutumia viungo, upofu, kufanga ganzi na kupoteza kumbukumbu.
Maambukizi
Kaswende huambukizwa endapo majimaji ya kwenye kidonda hugusana na mwili. Lakini pia huambukizwa kwa njia ya ngono, na hata kunyonya mate na kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Vipimo
Muda mfipi baada ya kupata maambukizi mwili hutengeneza kinga ya kupambana na wadudu wa kaswende. Hivyo hii kinga inaweza kupimwa maabara kwa kutumia kipimo maalumu. Wakati mwingine uchunguzi huwezwa kufanya kwa kuchukua majimaji kutoka kwenye kidonda.
Uhusiano kati ya kaswende na HIV
Kwakuwa mgonjwa wa kaswende anakuwa na vidonda ni rahisi kupata maambukizi ya HIV.
Matibabu.
Hakuna matibabu ya nyumbani yanayoweza kuponyesha huu ugonjwa. lakini unatibika kwa urahisi kwa kutumia antibiotics amabazo unaandika na daktari. Hivyo unapokuwa na dalili hizo ni vyema kuwahi hospitali,

No comments:
Post a Comment