TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU CALL: 0712 005 865 au EMAIL: dr.masua@paulmasua.com

Monday, September 26, 2016

Waathirika wa VVU kuanza kutumia dawa,baada ya kugundulika kuwa na maambukizi

Serikali imetoa mwongozo mpya unaelezea wakati wa kuanzisha dawa za kupunguza makali ya VVU na UKIMWI. Katika mwongozo huo serikali inaelekeza kuwa dawa hizo zianze kutolewa kwa mtu yeyote anayegundulika kuwa na maambukizi ya VVU bila kuangalia kiwango cha CD4+.

Hatua hiyo inafuatia mwongozo uliotolewa na Shirika la Afya duniani. Serikali  itaanza kutelekeza utaratibu huo mwezi October.

Tafiti zimeonyesha kuwa kuanza kutumia dawa mapema kuna faida zaidi kwa mgonjwa kuliko kusubiri kiwango cha CD4+ kushuka. Baadhi ya faida hizo ni kupunguza hatari ya maambukizi, kupunguza magonjwa nyemelezi pamoja na ugonjwa wa UKIMWI.

Hata hivyo utaratibu huu mpya unachangamoto kadhaa hasa kuongeza mzigo wa gharama kwenye sekta ya afya.

Monday, August 15, 2016

Namna ya kukadiria uzito wa mtoto kwa umri wake

Kwa kawaida mtoto anayezalia baada ya ujauzito kufikia ukomavu wa majuma 40 huwa na uzito unaokadiriwa kufikia 3.5kg. Hata hivyo uzito huu huongeza mara mbili mtoto anapofikia umri wa miezi  mitano na huwa mara tatu zaidi anapokuwa na mwaka mmoja.Hivyo basi mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja ana uzito unaokadiriwa kufikia 10kg.

Kuanzia mwaka 1 mpaka 6 , uzito wa mtoto huongeza kwa 2kg kila baada ya mwaka mmoja.  Hivyo mtoto mwenye miaka miwili ana uzito unaofikia 12kg, miaka mitatu uzito unaokadiriwa kuwa 14kg wakati wenye miaka 4 ,uzito unakuwa 16.

Watoto wenye umri kuanzia miaka 6 hadi 10 inakadiriwa kuwa huongeza 3kg kila baada ya mwaka mmoja.  Mfano mtoto mwenye umri wa miaka 7 anakadiriwa kuwa na uzito wa 23kg wakati mwenye miaka nane akiwa na uzito unaofikia 26kg

Tuesday, May 31, 2016

Mimba hatarishi ni nini?

Mimba hatarishi ni ujauzito ambao huatarisha au kutishia afya pamoja na maisha ya mama na mtoto(kichanga)

Nini husababisha mimba kuwa hatarishi?
Magonjwa au maradhi anayokuwa nayo mama kabla ya ujauzito 
Baadhi ya kina mama wana matatizo mengine ya kiafya kabla ya kushika ujauzito. Mfano maradhi ya shinikizo LA damu, kisukari na maambukizi ya VVU. Maradhi hayo hufanya ujauzito kuwa hatarishi

Monday, May 23, 2016

Kwa nini Wanawake Wajawazito hukatazwa kulala chali?

Wakati wa ujauzito hutokea mabadiliko kadhaa katika afya ya mwanamke.  Mabadiliko hayo husabishwa na uwepo wa mtoto kwenye mfuko wa uzazi.

Ujauzito unapofikia wiki 20 (mfuko wa  uzazi huwa usawa wa kitovu) na kuendelea uzito wa mtoto pamoja na ukubwa wa mfuko wa uzazi husababisha mgandamizo mkubwa kwenye mishipa mikubwa ya damu.  Mishipa hii hutoa damu kwenye moyo na kusambaza sehemu za chini za mwili na mshipa mwingine hutoa damu sehemu za chini za mwili na kuirudisha kwenye moyo.

Friday, April 22, 2016

CD4+ ni Nini?

CD4+ni nini?
CD4+ ni aina ya seli nyeupe za damu zinazohusika na kinga  dhidi ya magonjwa mbalimbali  na pia zinasaidia seli nyingine za kinga ya  mwili. CD4+   hushambuliwa na na VVU kwa sababu katika hizi seli virusi huzaliana. CD4+ hupungua taratibu hivyo na hivyo magonjwa nyemelezi huanza kushambulia na hata kusababisha kifo.

1.Kiwango cha kawaida cha CD4+ ni 1000. Mtu mwenye maambukizi ya VIRUSI VYA UKIMWI CD4+ hupungua kwa kiwango cha seli 60 kwa mwaka

Thursday, April 7, 2016

Tiba Mbadala ni salama kiasi gani?


Tiba mbadala maana yake ni tiba au matibabu ni mbadala wa matibabu ambayo yamethibitishwa na yenye ubora uliohakikiwa pamoja na usalama na nguvu za kutibu magonjwa mbalimbali. Maana nyingine ni kuwa ubora au uwezo wa kutibu wa tiba mbadala haujathibitika kitaalamu na pia usalama wake au madhara yake haviko wazi.

Wednesday, April 6, 2016

Je hutokea nini tangu kupata maambukizi ya VVU hadi kuugua UKIMWI?

Virusi vya UKIMWI huanza kuzaliana mara tu baada ya maambukizi ya awali hivyo kupelekea ugonjwa wa UKIMWI au hufubaa kwa muda kabla ya kuanza kuonyesha dalili za UKIMWI.

Kipindi hicho cha kufubaa (Chronic Latent Course) hupitia hatua tatu. Kipindi hiki huduma kwa wastani wa miaka nane, lakini inaweza kuwa chini ya mwaka mmoja na kati ya miaka 20 kabla ya kuugua UKIMWI.